2



Kwa ujumla tangawizi hustawi kwenye mwinuko kuanzia m 800 mpaka 1500 kutoka usawa wa bahari, kwa ujumla maeneo mengi inakostawi kahawa na tangawizi zinastawi.

Maandalizi ya mwanzo ya shamba kwaajili ya kulima Tangawizi
Maandalizi ya mwanzo ya shamba kwaajili ya kilimo cha Tangawizi
KUANDAA SHAMBA
Andaa Shamba lako mapema, katua/lima kuanzia miezi ya
April, may au June, ni vizuri ukaanzisha Shamba jipya au lilikaa bila kulimwa kwa miaka mitatu, Lainisha udongo miezi ya August au September na kuanzia November unaweza kuanza kupanda.
.
KUPANDA
Tangawizi hupandwa kwa kuivunja vunja kwa kufuatisha mbingili zake. Panda tangawizi kwa cm 30 kati ya shina moja na jingine na cm 45 mpaka 60 kati ya mstari mmoja na mwingine. Tumia  mbolea ya mboji au samadi na usitumie  mbolea za kemikali kupandia, Kg 1000 za tangawizi hupandwa katika hekta moja na unaweza kuvuna kuanzia tani 10 mpaka 25 inategemea ukubwa wa mbegu, urutubishaji, kiasi cha maji na palizi. Huchukua wiki mbili mpaka mwezi mmoja na nusu tangawizi Kuota. Inategemea kiasi cha maji na joto kwenye udongo, ni vizuri kuzitandaza tangawizi kwenye kivuli na kufunika na gunia na kuzimwagilia ili ziote kabla hujazikatakata kwa ajili ya kwenda kupanda. Palilia Mara tu Majani yanapoota na pandishia udongo kwenye mashina ili tangawizi itanuke vizuri.
MAGONJWA
Tangawizi haishambuliwi sana na magonjwa ila Mara chache hushambuliwa na kuvu (fungus).

Mkulima ameshika shina moja la Tangawizi lenye zaidi ya Kg 1
KUVUNA
Huchukua miezi 6 mpaka 18 kukomaa, inategemea mwinuko toka usawa wa bahari na mvua.
 Tangawizi haitaki maji yanayotuama kama vijaruba vya mpunga, maji yakituama kwenye shina la tangawizi kwa mda Fulani Majani ya tangawizi huwa ya njano na huanza kunyauka.
 Kuvuna Tani 10 kwa hekta moja ni kadirio la chini kabisa.. Kipindi soko linapokua zuri unaweza kupata kuanzia Mil 20 mpaka 60 kwa hekta moja, kuna wahindi ambao hununua tangawizi kwa wingi sana na wanaexport, wahindi hununua kg 1 kwa sh 3000, mpaka 3500 ukiuzia shambani
Uzuri tangawizi unaweza kusubiri soko zuri na ukauza kwa bei nzuri kwani zao hili hupanda bei haraka.
Watu wengi wanashindwa kuzalisha tangawizi kwa wingi kwa kukosa mitaji ya kununulia mbegu kwani mbegu zake ni gharama, hivyo unashauriwa kununua kg chache walau kg 200 ukapanda eneo dogo ili kuzĂ lisha mbegu ambazo utaweza kuzisambaza eneo kubwa, na kwa kulima eneo dogo unaweza kupata  uzoefu kupitia hapo na kujua kama  eneo ulilolima ni sahihi na linafaa kwa kilimo cha tangawizi.
 Sokoni tangawizi huuzwa sh 5000 mpaka 6000 kwa kg soko linapokua zuri, pia tangawizi kuna msimu hushuka bei mpaka sh 2000 kwa kg. Usikatishe tamaa pale  tangwizi inaposhuka bei mpaka sh. 1500, unaweza kusubiri kwa mda mfupi na kuuza tangawizi kwa bei nzuri sana kwa kuwa bei yake hupanda kwa haraka.

Mkulima wa Tangawizi Songea
HALI YA HEWA
Mimea hii husitawi katika maeneo  yenye joto la wasitani yaani haihimili hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu. Tangawizi hukua vizuri katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi.  Iwapo Tangawizi itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za sentigrade huchelewa kuota.
MVUA
Kwa upande wa mvua Tangawizi huhitaji kiasi cha mvua kati ya millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.
HALI YA UDONGO
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile  haihitaji udongo wenye  kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya udongo katika kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0.
 
 
MAKALA HII IMEANDALIWA NA MTAALAM NA MSHAURI WA MASUALA YA KILIMO,
KINOJA MAPIGANO,
+255768449499 , +255716964704 
S.L.P 5960 DSM.
kilimobiashara@gmail.com
Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

Post a Comment

 
Top